Home Simba SC SIMBA YAMUWEKA KANDO BEKI HUYU AMBAYE WANATAJWA KUIWINDA SAINI YAKE

SIMBA YAMUWEKA KANDO BEKI HUYU AMBAYE WANATAJWA KUIWINDA SAINI YAKE


WAKATI wakitajwa kuwa kwenye maboresho ya kikosi cha Simba kwa ajili ya msimu ujao na jina la nahodha wa Kagera Sugar, David Luhende likitajwa kuwa kwenye rada za vinara hao, Simba wameamua kuweka kiporo suala hilo.


Luhende ni miongoni mwa wazawa ambao wanafanya vizuri ndani ya uwanja akiwa ni beki namba moja kwa utoaji wa pasi.

 Ametoa jumla ya pasi saba za mabao na amefunga mabao mawili kwa mipira iliyokufa jambo ambalo linatajwa kuwavutia mabosi wa Simba.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa hawafikirii masuala ya usajili na badala yake wamewekeza nguvu kubwa kwenye mechi zao ambazo zimebaki.

“Tuna mechi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho huko nguvu zetu tumeziwekeza kwa sasa hivyo hayo masuala mengine ni suala la kusubiri,” amesema Rweyemamu.

Leo Simba ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting.

SOMA NA HII  KUHUSU SAKHO KUSEPA SIMBA...BARBARA AANIKA UKWELI WA MAMBO ULIVYO...SENEGAL 'WAMMAINDI' KUCHEZA LIGI YA TZ..