Home Habari za michezo KUHUSU SAKHO KUSEPA SIMBA…BARBARA AANIKA UKWELI WA MAMBO ULIVYO…SENEGAL ‘WAMMAINDI’ KUCHEZA LIGI...

KUHUSU SAKHO KUSEPA SIMBA…BARBARA AANIKA UKWELI WA MAMBO ULIVYO…SENEGAL ‘WAMMAINDI’ KUCHEZA LIGI YA TZ..


BAADA ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya goli bora la mwaka la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), nyota wa Simba, Pape Ousmane Sakho, ameingia katika rada za timu mbalimbali kwa ajili ya kumsajili raia huyo wa Senegal.

Goli ambalo limempa tuzo Sakho ni lile alilofunga dhidi ya ASEC Mimosas ndio limempatia ushindi huo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, alisema wamepokea maombi kutoka katika timu mbalimbali za ndani na nje ya Afrika zikionyesha nia ya kumsajili Sakho.

Barbara alisema maombi hayo yamepelekea yeye na nyota huyo kubakia Morocco ili kufikia uamuzi juu ya ofa hizo ambazo zimejitokeza.

“Simu zimekuwa nyingi sana kwa Pape, viongozi wa Senegal waliuliza kwanini anacheza Tanzania, walikuwa wanamwambia anapaswa kuondoka sasa na ni lazima aondoke akacheze nje ya hapa,” alisema Barbara.

Ofisa huyo aliongeza Simba itafanya uamuzi kwa kuzingatia malengo ya klabu lakini pia itaangalia maslahi ya mchezaji husika.

“Ukweli ni kwamba tumepokea ofa nyingi na jana (juzi) usiku baada ya tuzo watu wanatutafuta, wamemfuata mchezaji wanaomba vikao, leo (jana) wanaomba tuahirishe safari, mwisho wa siku wajibu wangu kama CEO lazima nilete kwa mabosi wangu ikiwamo mwenyekiti na rais ili maamuzi yao lazima yafanyike,” Barbara alisema.

Aliongeza bado Simba haijakamilisha mchakato wa usajili kwa maana hiyo uamuzi wa mwisho wa wachezaji watakaoitumikia klabu hiyo haujafanyika huku akisema wamepokea ofa mbili zinazomhitaji, Sadio Kanoute.

“Kumekuwa na mchakato makini unaoendelea katika klabu yetu, bado hatujafunga, hatujakamilisha usajili, haijajulikana kamili nani anaingia na nani anatoka, muda ukifika tutaweka wazi, kikubwa tutazingatia malengo ya klabu tuliyojiwekea,” Barbara aliongeza.

Taarifa ambazo zimepatikana jijini zinasema klabu ya zamani ya Mtanzania, Simon Msuva, Wydad Casablanca ya Morocco iko tayari kumnunua Sakho kwa dau la Sh. bilioni 1.8.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo, Sakho aliwashukuru Watanzania, mashabiki wa Simba na wachezaji wenzake wote wa klabu hiyo.

“Asanteni Watanzania, asanteni mashabiki wa Simba, asanteni wachezaji wote, nimefurahi sana,” alisema mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  UEFA YAMPANGA REFA MWENYE BAHATI NA MADRID KUCHEZESHA FAINAL YA LIVERPOOL vs MADRID...

Sakho ambaye katika fainali ya kuwania tuzo hiyo alishindana na Zouhair El-Moutaraji wa Wydad na Gabadinho Mhango wa Malawi alikabidhiwa tuzo yake na mkongwe, Jay Jay Okocha.