Home Habari za michezo UEFA YAMPANGA REFA MWENYE BAHATI NA MADRID KUCHEZESHA FAINAL YA LIVERPOOL vs...

UEFA YAMPANGA REFA MWENYE BAHATI NA MADRID KUCHEZESHA FAINAL YA LIVERPOOL vs MADRID…


Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la soka barani ulaya UEFA imemteua muamuzi Clement Turpin (39) kuchezesha mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA Champions league 2022 kati ya Liverpool na Real Madrid.

Fainali hiyo itapigwa katika uwanja wa Stade de France mjini Saint-Denis, nchini Ufaransa jumamosi ya mei 28 mwaka huu kuanzi majira ya saa tatu usiku.

Turpin ambaye ni mwamuzi wa kimataifa tangu mwaka 2010, anatazamiwa kuchezesha fainali yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani ulaya akiwa mwamuzi wa kati baada ya kuhudumu akiwa Mwamuzi wa nakiba katika mchezo wa fainali ya mwaka 2018, ambao uliwakutanisha pia Real Madrid na Liverpool na Madrid kutwaa ubingwa kwa kushinda magoli 3 kwa 1.

Turpin amechezesha mechi saba ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu hadi katika hatua ya mtoano, ikijumuisha mchezo wa robo fainali ya kwanza kati ya Chelsea FC na Real Madrid katika dimba la stanford bridge jijini London.

Turpin pia ndiye aliyechezesha mchezo wa fainali ya ligi ya Europa msimu uliopita uliowakutanisha Villareal na Manchester United, na Villareal kutwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati 11 kwa 10.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSIKIA MAYELE NDIYE MFALME BONGO...BALEKE KAKUNA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HILI..