Home Habari za michezo KISA USHINDI WA GOLI 4-1 WA YANGA JUZI…JEMEDARI SAID AWAGEUKA SIMBA…AWAPA ‘MAKAVU...

KISA USHINDI WA GOLI 4-1 WA YANGA JUZI…JEMEDARI SAID AWAGEUKA SIMBA…AWAPA ‘MAKAVU LIVE’ KUHUSU TABIA ZAO…

Jemedari saidi awananga Yanga SC

Mchambuzi maarufu wa Soka nchini, Jemedari Said amewashtukia baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakiponda ushindi wa Klabu ya Yanga wakidai kuwa ananunua mechi pasi na uthibitisho wa kauli hizo.

Kauli hiyo ya Jemedari inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Yanga kuichakaza vibaya Singida Big Stars hapo jana kwa kuifunga bao 4-1 katika Dimba la Mkapa.

“Hii Nchi ina watu wa ajabu sana, Yanga ambao ni mabingwa wa vikombe vyote vya ndani kushinda (4-1) dhidi ya Singida eti wamenunua mechi,, Simba kushinda (5-0) dhidi ya Mtibwa tena yenye Wachezaji (9) kimyaa hakuna aliyesema Simba wamenunua mechi.

“Kuna watu wa hovyo sana nchi hii. Golikipa wa Singida Khomein alikuwa na mapungufu ndio lakini alifanya mapungufu makubwa zaidi kwenye mchezo dhidi ya Simba yakasababisha Peter Banda akamfunga kizembe kabisa lakini hakuna aliyesema Simba kanunua mechi.

“Huu ni ujinga haupaswi kuachwa hivihivi bila kukemewa,, Kwa hiyo Yanga hii haina uwezo wa kumfunga Singida ?.. Ni ujinga tu,” amesema Jemedari Said.

SOMA NA HII  MAKAMBO ANA JAMBO LAKE, MUGALU NAYE PIA NI NDANI YA SPOTI XTRA JUMANNE