Home Uncategorized AZAM FC: TUPO TAYARI KWA MSIMU MPYA WA 2020/21

AZAM FC: TUPO TAYARI KWA MSIMU MPYA WA 2020/21


AGREY Morris, nahodha wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6.

Tayari Azam FC yenye maskani yake Chamazi imeshakamilisha masuala ya usajili na utambulisho wa wachezaji wake wapya kwa mashabiki kupitia tamasha lao la Azam Festival lililofanyika Agosti 23.

Kwenye kilele cha Azam Festival ilicheza na Namungo FC ya Lindi ambapo ilishinda mabao 2-1. Itafungua pazia na Polisi Tanzania, Septemba 7, Uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00 usiku.

Moris amesema:-“Kikosi kipo imara kwa sasa na kila mchezaji yupo tayari kwa ushindani kwa kuwa maandalizi ni mazuri na morali ya wachezaji ni kubwa.

“Kwa sasa kitu pekee kilichobakia ni sisi wachezaji kuhakikisha tunajitoa na tunafanikiwa msimu mpya wa 2020/2021.”

Moris, Agosti 24 aliongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kukitumikia kikosi hicho hivyo bado yupoyupo ndani ya kikosi hicho.


SOMA NA HII  EXCLUSIVE, YANGA WAIGOMEA VODACOM