Home Uncategorized BREAKING NEWS: KILOMONI “NINJA” AACHIWA NA POLISI NA KUENDELEA NA MKUTANO WA...

BREAKING NEWS: KILOMONI “NINJA” AACHIWA NA POLISI NA KUENDELEA NA MKUTANO WA WAANDISHI




Mwanachama maarufu wa Simba, Hamisi Kilomoni ameachiwa huru bada ya kukamatwa na jeshi la Polisi kutokana na kufanya mkutano bila ya kuwa na kibali.


Mzee Kilomoni alikamatwa na kuepelekwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay ambako alishikiliwa kwa muda.


Hata hivyo, baadaye Kilomoni aliachwa huru na kurejea nyumbani kwake katika eneo la Block 41, si mbali sana na kituo cha Oysterbay na kuendelea na mkutano.


Taarifa zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa Mzee Kilomoni anaendelea na mkutano huo wa waandishi wa habari kuhusiana na klabu ya Simba.

SOMA NA HII  YANGA WACHEKELEA SAPOTI YA MDHAMINI KUMWAGA MKWANJA