Home Uncategorized YANGA WACHEKELEA SAPOTI YA MDHAMINI KUMWAGA MKWANJA

YANGA WACHEKELEA SAPOTI YA MDHAMINI KUMWAGA MKWANJA


JUMA Abdul nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa mdhamini wao GSM amewaongezea nguvu ya kufanya mazoezi wakiwa nyumbani kutokana na kupewa fursa ya kufanya manunuzi kwenye duka la michezo lililopo Mlimani City.

Abdul amesema kuwa vifaa hivyo walivyonunua vitawasaidia kufanya mazoezi nyumbani kwa umakini huku wakichukua tahadhari ya Virusi vya Corona.

“Fursa ya kufanya manunuzi kwenye duka la mdhamini wetu wetu tumeifurahia na imetufanya tuwe na furaha zaidi kwani itatufanya tuendelee kufanya mazoezi nyumbani na kuendelea kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona,” amesema.

SOMA NA HII  VIDEO: MBELGIJI AZUNGUMZIA HATMA YA MOLINGA