Home kimataifa ARGUERO ANATAKA KUJIUNGA NA BARCELONA

ARGUERO ANATAKA KUJIUNGA NA BARCELONA


 SERGIO Arguero, mshambuliaji wa kikosi cha Manchester City imeelezwa kuwa amewaambia watu wake wa karibu kwamba anataka kujiunga na Klabu ya Barcelona.

Tayari imewekwa wazi kwamba mshambuliaji huyo raia wa Argentina hatakuwa kwenye kikosi hicho msimu utakapomeguka kwa sababu amemaliza mkataba na hataongeza mwingine.

Habari zimeeleza kuwa nyota huyo ambaye alicheza ndani ya La Liga akiitumikia Klabu ya Atletico Madrid anahitaji kurejea tena kwenye ligi hiyo kubwa ya Hispania.

Aguero, raia wa Argentina mwenye miaka 32 amekuwa akihusishwa kujiunga na Chelsea pamoja na Manchester United ambazo zinahitaji kumuona nyota huyo akibaki ndani ya Premier League.

SOMA NA HII  SIMBA TENAA...WAMKOSA MCHEZAJI MWINGINE WA MAANA KWA 'KUJIUMA UMA KUFUNGUA POCHI'.....