Home Habari za michezo SIMBA TENAA…WAMKOSA MCHEZAJI MWINGINE WA MAANA KWA ‘KUJIUMA UMA KUFUNGUA POCHI’…..

SIMBA TENAA…WAMKOSA MCHEZAJI MWINGINE WA MAANA KWA ‘KUJIUMA UMA KUFUNGUA POCHI’…..

Habari za Simba

Aliyekuwa Kiraka wa Klabu ya Mtibwa Sugar, Nickson Kibabage amekamilisha usajili wa kujiunga na na Klabu ya Singida Big Stars Kwa Mkataba wa Miaka mitatu kama Mchezaji huru.

Kibabage ametimkia Mkoani Singida, baada ya Uongozi wa Mtibwa Sugar kukubali kumuachia kwa makubaliano maalum na Viongozi wa Singida Big Stars, ambao wamekubali kununua sehemu ya mkataba wake iliyokuwa imesalia klabuni hapo.

Kwa mantiki hiyo Kibabage ambaye aliwahi kucheza soka nchini Morocco akiwa na Klabu ya DifaĆ¢ El Jadidi na baadae kutolewa kwa mkopo Youssoufia Berrechid, muda wowote atatangazwa ndani ya Singida Big Stars.

Kibabage mweye umri wa miaka 22 alikuwa anawaniwa pia na Miamba ya Soka ya Tanzania Simba SC lakini ofa ya Klabu hiyo ya Msimbazi ilikuwa ni kumsajili kinda huyo mwishoni Mwa Msimu Baada ya Mkataba wake na Mtibwa kumalizika.

Usiku wa kuamkia jana Kibabage aliwaaga rasmi Mashabiki wa Mtibwa Sugar kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram: Nipende kutoa shukrani zangu kwenu familia yangu ya muda wote @mtibwaofficial tumeanza na wakati mzuri kwenye huu msimu nawashukuru kwa upendo mlionionesha kijana wenu naimani tutakutana wakati mwengine tena mwenyezi Mungu azidi kuwapa moyo huo huo UNITED WE STAND.

SOMA NA HII  SUALA LA KRAMO KUUMIA TENA ...BOSI SIMBA AVUNJA UKIMYA...UCHUNGUZI KUFANYIKA...