Home Habari za michezo ISHU YA BASI LA SIMBA KUTOONEKANA….UKWELI UKO HIVI….BARBARA ALIHUSIKA A-Z…

ISHU YA BASI LA SIMBA KUTOONEKANA….UKWELI UKO HIVI….BARBARA ALIHUSIKA A-Z…

Basi la Simba

Kitendo cha timu ya Simba kutotumia magari yao kwenye safari zake za hapa na pale pamoja na kwenda nayo uwanjani kwenye mechi kimeanza kuwashangaza wengi huku wakiwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni Simba ikiwa inaenda uwanja wa Ndege kwa ajili ya kusafiri kwenda Mbeya walionekana wakiwa kwenye gari dogo la kukodi aina ya (Coaster), badala ya magari ambayo wamepewa na wadhamini wao.

Simba ilisaini mkataba wa miaka minne na moja ya kampuni ya uuzaji na kukodisha magari mwaka jana, Septemba 24 na kuwapa magari matatu kwa ajili ya timu ya wakubwa, vijana na wanawake.

Kabla ya timu kupewa magari hayo bado ilikuwa na gari la wadhamini wake wa zamani sawa na Yanga walilopewa Septemba 12,2012, ambapo inadaiwa lilipelekwa kwa timu yao ya vijana baada ya kupata gari jipya.

Kinachoshangaza ni kuona timu hiyo ikiwa inakodi magari kwani licha ya kwenda uwanja wa ndege kwa gari ya kukodi, walifanya hivyo tena kwenye mechi yao dhidi ya Coastal Union ambapo walikodi gari hadi Tanga.

Ulipotafutwa uongozi wa timu hiyo na kutaka kufahamu nini kinachoendelea baada ya magari hayo kukosekana kwa muda mrefu.

Akizungumzia suala hilo Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema magari yao hayaonekani kwa sababu yako gereji na sio kama ambavyo watu wamekuwa wakizungumza kuhusu kushikiliwa kwa sababu za kukiuka mikataba.

“Wenye mamlaka ya kuzungumzia hayo ni viongozi wa Simba na mimi niseme tu wazi kwa mashabiki wetu kwamba mabasi yapo gereji pale Vingunguti kwenye makao makuu (jina limehifadhiwa), na yatakapokamilika kufanyiwa ukarabati mtayaona.”

Hata hivyo, kauli hiyo inazua utata kwa sababu gari moja la zamani (kubwa) halikuwa kwenye mkataba wa kampuni hiyo ambayo inawadhamini kwa sasa na wala halipo gereji.

Awali wakati mkataba wa magari hayo unasainiwa, Mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema mkataba huo una thamani ya Sh800 kwa kupewa mabasi matatu kwa timu zao tatu na watakuwa wanawasaidia katika mambo mengine ya msingi.

“Wameona wanaweza kutangaza bidhaa zao kupitia Simba na walifanya majaribio ya hilo kupitia kwa mlezi wetu wa Simba Queens, Fatema Dewji ambaye kwa kipindi cha miezi minne tumeona thamani kubwa,” anasema Barbara na kuongeza;

“Fatema akaona kwa nini asijiongeze zaidi kwa ajili ya timu zetu nyingine kufanyiwa uwekezaji na amefanya kazi kubwa kwani gari moja si chini ya Sh460 milioni na Simba tumepata bure kazi yetu ni kumuweka dereva na mafuta tu,” anasema Barbara.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA AZIZ KI KUTUA YANGA IMEFIKIA HATUA HII AISEE...YACOUBA ATAJWA KUTIA MKONO...