Home Azam FC AZAM FC WABAINISHA NAMNA JAMBO LAO LITAKAVYOTIMIA

AZAM FC WABAINISHA NAMNA JAMBO LAO LITAKAVYOTIMIA

 


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa bado hesabu zao katika kuwania kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara zinaendelea kwani wana kikosi imara ambacho kinarejea kwenye ubora ule wa awali.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ilianza mzunguko wa kwanza kwa kufanya vizuri ambapo iliongoza ligi mpaka raundi ya 7 kisha hapo mambo yalianza kubadilika taratibu na kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.

Kwa sasa ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 28 ina pointi 54, kinara ni Simba mwenye pointi 58 na amecheza jumla ya mechi 24, nafasi ya pili ipo mikononi mwa Yanga wenye pointi 57 baada ya kucheza mechi 27.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa na mechi mkononi pamoja na mipango waliyonayo bado inawapa nafasi ya kuamini kwamba jambo lao linakwenda kutimia.

“Huu ni mchezo wa mpira na inaonesha kwamba mzunguko wa pili ushindani ni mkubwa, ikiwa ipo hivyo basi hakuna namna kusema kwamba hatuna nafasi ya kutimiza jambo letu.

“Ukiwatazama wale wanaoongoza ligi wametuzidi pointi nne na wana mechi mkononi, sawa hilo lipo wazi ila nasi pia bado tuna mechi za kucheza hivyo tukishinda zetu wao wana kazi pia ya kupambana kushinda mechi zao.

“Kwa maana hiyo bado mbio za ubingwa zipo wazi na jambo letu tunaamini kwamba linakwenda kutimia kwa kuwa timu imerejea kwenye ule ubora wa awali,” amesema.

Mchezo uliopita Azam FC ilishinda bao 1-0 dhidi ya Azam FC na bao la ushindi lilifungwa na Prince Dube ambaye ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 12 anafuatiwa na Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 11.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF...KOCHA MFARANSA AWAPA MASHARTI HAYA AZAM FC...WAKISHINDWA IMEKULA KWAO...