Home Uncategorized KMC YAGOMEA KUSHUKA DARAJA, YATAJA MBINU WATAKAZOTUMIA KUBAKI

KMC YAGOMEA KUSHUKA DARAJA, YATAJA MBINU WATAKAZOTUMIA KUBAKI


UONGOZI wa KMC umesema kuwa utapambana kwa nguvu zote kuhakikisha timu inabaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2019/20.


KMC ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 29 kibindoni ina pointi zake 33.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwary Binde amesema kuwa wapo tayari kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki ili kujikusanyia pointi nyingi zaidi.

“Kweli hatukuanza vizuri hilo lipo wazi ila kwa sasa tupo sawa kutokana na kikosi kuwa na muunganiko mzuri hivyo tutapambana kuona timu inabaki ndani ya ligi,” amesema.

Jana KMC ilimenyana na Azam FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na kutoshana kwa kufungana bao 1-1.
SOMA NA HII  TUNDAMAN KUACHIA NGOMA SOON! “SIWEZI KUWATUNGIA WIMBO YANGA” – VIDEO