Home Habari za michezo HAPA NAPO PANAHITAJI AKIBA YA MANENO

HAPA NAPO PANAHITAJI AKIBA YA MANENO

Piga Bao

Wikiendi hii Ligi ya Championship inaingia katika raundi ya 13 ambapo zitabakia raundi mbili tu ili nusu ya kwanza imalizike na baada ya hapo zitabakia raundi 15 za nusu ya pili na ya lala salama.

Msimamo wa ligi hiyo unaongozwa na KenGold ya Mbeya ambayo ina pointi 26 sawa na Mbeya Kwanza iliyopo nafasi ya pili huku TMA ya Arusha ikiwa katika nafasi ya tatu na Pamba inashika nafasi ya nne.

Kwa mujibu wa kanuni, timu mbili zitakazoongoza msimamo wa ligi hiyo mwishoni mwa msimu zitapanda Ligi Kuu msimu ujao na mbili zitakazofuata zitacheza mtoano kutafuta timu moja ambayo itakutana na timu moja ya Ligi Kuu kutafuta nafasi ya kupanda daraja .

Kitendo cha kuwepo katika nafasi nne za juu hadi nusu ya kwanza inapokaribia kumalizika kunaziweka KenGold, Mbeya Kwanza, TMA na Pamba katika nafasi nzuri ya kusaka nafasi mbili za kupanda Ligi Kuu msimu ujao pamoja na ile ya kucheza mechi za mtoano.

Hata hivyo, ni mapema sana kuzipa uhakika mkubwa timu hizo kumaliza katika nafasi nne za juu mwishoni mwa msimu kwani nusu ya pili huwa na matokeo mengi ya kushangaza na kushtukiza ambayo yanaweza kufanya watu wabaki vinywa wazi.

Ukiangalia msimamo wa ligi hiyo ulivyo hivi sasa utaona ni kwa namna gani timu hazijapishana kwa idadi kubwa ya pointi huku zikiwa zimebaki raundi 18 kwa kila timu ambazo zinaweza kubadili hali ya mambo hapo baadaye.

Unaweza kushangaa kuona timu ambayo leo hii inapambana kuhakikisha haishuki daraja, dakika za jioni wakati ligi inakaribia kumalizika ikaonekana ipo katika vita ya kumaliza katika nafasi nne za juu na mara nyingi hilo limeshajitokeza.

Kimsingi timu zinapaswa kufahamu kwamba raundi 18 ambazo zimebakia ndio ngumu na zinazohitaji umakini na maandalizi bora zaidi kulinganisha na hizo 12 zilizopita.

SOMA NA HII  YALIYOMKUTA ACHRAF HAKIMI...YAMNYEMELEA C.RONALDO...ISHU NZIMA IKO HIVI