Home Habari za michezo KISA MAKUNDI YA CAF…AHMED ALLY NA ALLY KAMWE WAANZA ‘SHIT’ ZAO MAPEMA…

KISA MAKUNDI YA CAF…AHMED ALLY NA ALLY KAMWE WAANZA ‘SHIT’ ZAO MAPEMA…

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), jana lilichezesha droo ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wawakilishi wa Tanzania, Yanga SC na Simba SC, wamewafahamu wapinzani wao.

Baada ya makundi kupangwa, Simba wametamba kwamba watatoboa hatua hiyo, huku Yanga ikiliachia benchi la ufundi chini ya Kocha Nasrddine Nabi kumaliza kazi.

Katika droo hiyo, Yanga imepangwa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika na timu za Union Sportive Monastery ya Tunisia ambako watarudi huko kucheza baada ya kuwaondoa Club Africain hatua ya Play-Off ya michuano hiyo. Zingine ni TP Mazembe ya DR Congo na Real Bamako ya Mali.

Akizungumzia kundi hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, alisema mara baada ya droo hiyo kuchezeshwa, haraka maandalizi na mikakati ya michuano hiyo imeanza.

Kamwe alisema, walijipanga kukutana na timu yoyote hatua ya makundi, hivyo wanaziheshimu timu walizopangwa nazo, lakini malemngo yao ni kufika mbali.

“Kabla ya droo kuchezeshwa tulijipanga kukutana na timu yoyote tutakayopangwa nayo, kwani tupo vitani tumejiandaa kupambana na mpinzani yeyote.

“Benchi letu la ufundi lilikuwa mubashara kufuatilia droo hiyo, hivyo tunaamini watajipanga vema kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu msimu huu,” alisema Kamwe.

Makundi mengine ya Kombe la Shirikisho ni; KUNDI A: USM Alger, Morumo Gallants, Al Akhdar na FC Lupopo. Kundi B: ASEC Mimosas, Diables Noirs, Rivers United na DC Motema Pembe na Kundi C: Pyramid FC, Asko de Kora, Future na AS Far Club.

Nao wawakilishi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC, wameangukia Kundi C lenye timu za Raja Casablanca ya Morocco, Horoya AC (Guinea) na Vipers SC (Uganda).

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alizungumzia kundi hilo na kusema: “Sisi ni wakubwa, hivyo tulitarajia kukutana na wakubwa wenzetu katika droo hii iliyochezeshwa.

“Hivyo basi tunaamini benchi la ufundi limeiona droo hiyo, watajipanga kwa ajili ya mapambano ili kufikia malengo yetu.

“Wanasimba waondoe hofu, tunakwenda katika usajili, hivyo tutafanya usajili bora utakaoendana na ukubwa wa mashindano tunayoshiriki, naamini tutatoboa,” alisema Ahmed.

Makundi mengine ni; Kundi A: Petroleos, JS Kabylie, AS Vita Club na Wydad Casablanca. Kundi B: Mamelod Sundowns, Al Hilal, Cotton Sports na Al Ahly ya Misri na Kundi D: Zamalek, CR Belouizdad, Al Merikh na Esperance.

SOMA NA HII  MERIDIANBET WATEKELEZA AGIZO LA DR SAMIA KWA VITENDO...WASHUSHA NEEMA KWA T.Z.K FC..