Home Uncategorized STERLING KUFIKIA KIWANGO CHA MESSI?

STERLING KUFIKIA KIWANGO CHA MESSI?


Huku akiwa alifunga magoli 17 msimu uliopita , matatu katika mechi moja msimu huu- Raheem Sterling yuko tayari kwa msimu mwengine bora mwaka huu.

Mshambuliaji huyo wa Man City alikuwa na kampeni ya kipekee 2018-19 , akichaguliwa na waandishi kuwa mchezaji bora, mchezaji mwenye umri mdogo wa mwaka pamoja na kushirikishwa katika timu bora ya mwaka baada ya magoli yake kuisaidia timu yake kushinda taji la ligi ya Premia katika msimu wa pili mfululizo ambao pia waliweza kushinda mataji matatu.

Pia amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Garry Southgate akitajwa kuwa mchezaji maalum na mkufunzi wake Pep Guardiola na akiwa na umri wa miaka 24 miaka yake bora iko siku zijazo.

Katika kipindi cha BBC Radio 5 siku ya Jumatatu usiku – swali liliulizwa iwapo Sterling anaweza kuwa na msimu kama ule wa Messi – mshindi mara tano wa taji la Ballon d’Or na mfungaji mabao 30 na zaidi kila msimu ambaye kila mtu anaweza kujivunia.

Je ana malengo ya kufikia kiwango cha Messi?
Sterling alifunga magoli 25 katika mashindano yote msimu uliopita – yakiwa ndio mabao mengi aliyowahi kufunga katika msimu mmoja na aliendeleza msururu huo wa magoli kwa kufunga hat-trick katika mechi ambayo City iliibuka mshindi kwa magoli 5 wakicheza dhidi ya West Ham siku ya Jumamosi.

Akiwa na umri wa miaka 24 na siku 245 – Sterling alicheza na kutoa mchango kama ule wa Messi wakati mshambuliaji huyo wa Argentina alipokuwa na umri kama huo.

Sterling na Messi wakiwa na umri wa miaka 24 na siku 245 – Takwimu zao zinasemaje?

Mchezaji Mechi Dakika alizocheza Magoli Usaidizi wa magoli
Sterling 322 23,739 96 68
Messi 310 23,725 223 90

Tofauti iliopo kuhusu kiwango cha usaidizi wa kila mchezaji alichochangia katika wakati huo sio mkubwa – 90 kwa Messi ikilinganishwa na Sterling aliyekuwa na 68 – lakini ni ufungaji wa magoli mengi wa Messi ambao unamfanya kuwa mchezaji wa kipekee.

Huku Sterling akijishasha kwa kufunga magoli 25 msimu uliopita, magoli machache yaliofungwa na Mesi katika misimu yake 11 ni magoli 38.

Kwa Sterling kulinganishwa na Messi atalazimika kuongeza kiwango chake cha magoli maradufu.


“Raheem anaendelea kuimarika’ , alisema aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright akizungumza na BBC Radio 5 Live.

”Ni hodari sana jinsi anavyocheza na na kutamba na mpira na ufungaji wake ni mziuri zaidi. Ni rahisi kumuona mtu kama Raheem akimaliza na magoli kati ya 35 – 40 msimu huu kutokana na jinsi anavyocheza , fursa zinazotengezwa na Man City na jinsi anavyofunga magoli”.

Je Guardiola anaweza kuimarisha kiwacho cha Sterling na kufikia kile cha Messi?
Wakati Manchester City ilipomsaini Sterling kutoka Liverpool 2015 kwa dau la £49m, alikuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Uingereza.

Thamani yake ilitokana na shinikizo nyingi kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 20 na pengine haishangazi ni kwa nini Sterling hakuweza kuonyesha mchango wake aliotaka kutoa.

Lakini mtu mmoja ambayo hakuwa na wasiwasi naye ni mkufunzi Pep Guradiola.

Msimu wa 2016, wakati Sterling alipokuwa na msimu mbaya wa Ulaya ambapo alitolewa baada ya kipindi cha kwanza akiichezea England dhidi ya Wales kufuatia kipindi kibaya cha kwanza, alipokea ujumbe katika simu yake uliosema: ”Usijali najua wewe ni mchezaji mzuri, Utakaponifanyia kazi, nitakupigania”.

Ujumbe huo ulitoka kwa mkufunzi wake mpya wa klabu ambaye alimtambua Sterling kama mchezaji mwenye kipaji cha kuwa mchezaji bora sawa na Messi.

Katika msimu wake wa pili akishirikiana na Guardiola, Sterling alifunga magoli 23 – ikiwa ni mara mbili ya magoli aliyofunga katika misimu yake sita aliyocheza soka ya kulipwa.

Kama Sterling, ufungaji magoli wa Messi kabla ya kucheza chini ya ukufunzi wa Guardiola ulikuwa mzuri lakini sio bora – alifunga magoli 16 katika kipindi cha msimu wa 2007-08.

Lakini msimu uliofuata aliongezaa idadi hiyo na kufikia 38.

Kwa Sterling kuweza kujumuishwa na kulinganishwa na Messi idadi yake ya magoli itahitaji kuimarika zaidi.

Uimarikaji huo uliambatana na hatua ya Guardiola kumchezesha Messi kama mshambuliaji wa katikati na pia ameweza kumchezesha Sterling katikati katika mechi ya maandalizi ya msimu huu ambapo Sterling alifunga magoli matano.

”Kwa mkufunzi kama Pep hatakua na nafasi ya kupumzika”, Wright aliongezea.

”Amejitahidi vilivyo na imani yake imeongezeka kwa kwa kile ambacho amekuwa akifanya katika mazoezi. Sasa atakuwa akivunjika moyo kwa kufunga magoli matatu na kushindwa kufunga goli moja zaidi kwa sababu hilo ndio lengo lake sasa” . Anataka kuongeza idadi ya magoli yake.

‘Ni mchezaji ambaye ni moto wa kuotea mbali’
Huku ukufunzi wa Guardiola ukiwa umesaidia kuimarika kwa Sterling, kitu muhimu ni kuimraika kwa mafikra yake.

Mshambuliaji huyo amekabiliwa na ukosoaji mkubwa katika mchezo wake wa soka kufikia sasa kutoka kwa mashabiki na vyombo vya habari.

Lakini amefanikiwa kuwanyamazisha kwa kuendelea kujiimarisha kama mchezaji na kuwakosoa wakosoaji wake.

Kiungo wa kati wa West Ham Jack Wilshere amefanikiwa kucheza na Sterling England lakini alikua mpinzani wa mchezaji huyo siku ya Jumamosi.

”Nadhani ni mchezaji mzuri sana na alikuwa mchezaji mzuri sana mwaka uliopita. Inaonyesha tabia yake baada ya kombe la dunia 2014 na kua mmoja wapo wa wachezaji bora katika ligi mwaka huu”.

SOMA NA HII  ALIYEMPELEKA SIMBA MORRISON YAMKUTA