Home Uncategorized SANCHEZ AWAGEUZIA KIBAO MAN UNITED, TETESI KIBAO ZA SOKA DUNIANI HIZI HAPA...

SANCHEZ AWAGEUZIA KIBAO MAN UNITED, TETESI KIBAO ZA SOKA DUNIANI HIZI HAPA LEO


Alexis Sanchez anakataa kuondoka Manchester United msimu huu, pamoja na kwamba kocha Ole Gunnar Solskjaer kutishia kumfanya kuwa mchezaji wa akiba ikiwa atasalia na timu hiyo. Roma inatafuta wachezaji wengine. (Sun)

Hatahivyo, timu ya Serie A, AC Milan, Juventus na Napoli bado wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Chile, 30. (Mail)

Real Madrid imekataa ombi la Paris St-Germain kumjumuisha Vinicius Junior,19, katika ofa ya kumnyakua mshambuliaji wa Brazil Neymar,27. (AS)

Mbali na Vinicius, PSG wanapendelea Real wamjumuishe kiungo wa croatia Luka Modric,33 na kiungo wa Brazil Casemiro,27, kumpata Neymar. (Marca)

Neymar alikuwa mazoezini mwenyewe siku ya Jumatano, ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapouzwa.(Esporte Interactivo, via Mundo Deportivo – in Spanish)

Kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza bado kujiunga na PSG ikiwa hatakuwa sehemu ya ofa ya Neymar. (Goal)

Beki wa kati wa Manchester United Victor Lindelof, 25, anajiandaa kusaini mkataba mpya kwa ongezeko la mshahara mbali na pauni 75,000 alizokuwa akipata kwa wiki. (Aftonbladet – in Swedish)

Bayern Munich huenda wakafufua nia yao ya kumnasa winga wa Manchester City, Leroy Sane, ingawa mchezaji huyo, 23, ana jeraha la mguu, litakalo mfanya kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba. (Bild – in German)

Mshambuliaji wa Marseille na Italia Mario Balotelli,29, anajiandaa kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Brescia baada ya kukataa ofa ya Flamengo ya Brazil. (Guardian)

Flamengo bado wana matumaini ya kubadili msimamo wa Balotelli, baada ya kukubali ombi lake la kumsajili kaka yake Enock kucheza katika moja kati ya timu zao nyingine (Gazzetta dello Sport – in Italian)

SOMA NA HII  YANGA YAWAOMBA MASHABIKI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA