Home Uncategorized MWADUI KUIKOMALIA GEITA FC, YAGOMA KUSHUKA MAZIMA TPL

MWADUI KUIKOMALIA GEITA FC, YAGOMA KUSHUKA MAZIMA TPL

MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC,ambaye ni kinara wa utupiaji mabao kwa wazawa ndani ya ligi kuu msimu wa 2018/19 Salim Aiyee amesema kuwa watapambana kupata matokeo kwenye mchezo wao wa mwisho ili kubaki kwenye ligi.

Mwadui FC inacheza playoff na Geita, Juni 8 uwanja wa Mwadui ikiwa ni mchezo utakaoamua nani abaki ligi kuu ama apande wakiwa na kumbukumbu ya kutoshana nguvu mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini kwa kutoka suluhu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aiyee amesema kuwa nguvu kubwa kwa sasa ni kwenye mchezo wa marudiano ambao utakuwa ni zaidi ya fainali.

“Mchezo wetu wa mwisho lazima tupambane makosa ya mwanzo mwalimu ameyafanyia kazi hivyo tutatumia vema uwanja wa nyumbani, itakuwa ni zaidi ya fainali” amesema Aiyee mwenye mabao 18.

SOMA NA HII  HAWA HAPA NI MWENDO WA SABASABA NDANI YA LIGI KUU BARA