Home Uncategorized YANGA YAWAOMBA MASHABIKI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

YANGA YAWAOMBA MASHABIKI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amewaomba mashabiki kuendelea kufanya dua ili hali irejee kama zamani.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.

Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa na Serikali Machi 17 Yanga ilikuwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 27.

Morrison amesema:-“Tuendelee kumuomba Mungu maisha ya kawaida yarejee baada ya hili janga la Corona na turudi kufanya kazi ili mashabiki na wapenda soka wafurahie kazi yetu.

“Kwa sasa ninachukua tahadhari nikiwa nyumbani pia ninapeda kuona mashabiki pia wakichukua tahadhari kwani janga hili lipo na Virusi ni hatari,” .

SOMA NA HII  KOCHA MTIBWA AIBUKIA IHEFU