Home Habari za michezo DUH…UNAAMBIWA ILIBAKI HIVI TU…HUYU KOCHA WA ZAMAN WA SIMBA ARUDI TENA BONGO...

DUH…UNAAMBIWA ILIBAKI HIVI TU…HUYU KOCHA WA ZAMAN WA SIMBA ARUDI TENA BONGO MSIMU HUU…


Jana Coastal Union imemtambulisha Mkenya, Yusuf Chipo kuwa kocha mkuu wake kwa mkataba wa mwaka mmoja akichukua mikoba ya Juma Mgunda aliyetimkia Simba lakini nyuma ya dili hilo kukiwa na sinema ya aina yake.

Awali Uongozi wa Coastal ulifanya mazungumzo na aliyewahi kuwa kocha wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic ili kuja kuwanoa Wana Mangushi na kukubaliana kumshusha tena Bongo lakini shida ikaja kwenye mshahara akitaka Sh9 milioni kwa mwezi.

Baada ya kuwaambia hivyo uongozi wa Coastal ulikaa kikao cha ghafla na kutafakari ofa hiyo na mwisho kuamua kuachana naye katika dakika za mwisho na kugeukia kwa Chipo aliyekuwa akiinoa Pamba.

“Jina la kwanza na lilofanyiwa kazi ilikuwa ni Goran lakini hata la Chipo lilikuwa kwenye mipango kwani ni kipenzi cha mashabiki wetu hivyo tulivyoshindwa kumpata Goran ikabidi tumchukue huyu.” alieleza moja ya viongozi wa juu wa Coastal.

Haikuwa ngumu kwa Chipo kujiunga tena na Coastal kwani aliwahi kuinoa timu hiyo miaka ya nyuma lakini pia alipewa maslahi makubwa zaidi ya aliyokuwa akiyapata Pamba.

SOMA NA HII  HIZI HAPA SIKU 109 ZA MBRAZILI NDANI YA SIMBA SC....WALIOSEMA HAWEZI WAKIMBIA KIMYA KIMYA...