Home Uncategorized MAMA ASITISHA MKATABA WA AJIBU SIMBA, AMBAKISHA YANGA FC

MAMA ASITISHA MKATABA WA AJIBU SIMBA, AMBAKISHA YANGA FC


UONGOZI wa Yanga upo kwenye taratibu za mwisho za kumbakisha kiungo wake mshambuliaji, Ibrahim Ajibu huku mama yake akihusishwa.

Ajibu anaelezwa kumalizana na Simba akisaini dau la Shilingi Milioni 100 na tayari ametanguliziwa kishika uchumba cha Shilingi Milioni 20 ili asaini mkataba miaka miwili.

Akizungumza na Championi Jumatanio, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa wapo kwenye taratibu za mwisho za usajili huo baada ya yeye mwenyewe kuonyesha nia ya kutaka kubaki Jangwani.

Mwakalebela alisema, familia yake chini ya mama yake imeonekana kuvutiwa na mafanikio na maendeleo aliyoyapata akiwa na Yanga na kumshauri aendelee kubaki kwa kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili.

“Ajibu ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye ripoti ya kocha wetu Zahera ambaye yeye amependekeza tumbakishe katika kukiimarisha kikosi chetu.

“Tupo kwenye mazungumzo naye Ajibu pamoja na familia yake ambayo inataka kumuona akiendelea kuichezea Yanga afikie malengo mazuri.

“Hivyo, tunakamirisha taratibu za mwisho ambazo za kawaida kati ya viongozi na mchezaji mwenyewe, lakini kama tukiona tunashindwa kufikia maamuzi mazuri na yeye, basi tutamuacha tukisubiria mamuzi yake ya kuondoka au kubakia Yanga,”alisema Mwakalebela.

SOMA NA HII  SIMBA YAWAITA MASHABIKI,KICHAPO MBELE YA PRISONS CHAWAPA HASIRA