Home Uncategorized MOURINHO ANUKIA KUREJEA CHELSEA

MOURINHO ANUKIA KUREJEA CHELSEA


IMEELEZWA kuwa vuguvugu la kumtafuta meneja ndani ya kikosi cha Chelsea kwa sasa linamhusisha Jose Mourinho ambaye amewahi kukinoa kikosi hicho kwa mafanikio kabla ya kupigwa chini.

Kwa sasa Chelsea wanatafuta meneja kutokana na Maurizio Sarri kuhusishwa kujiunga na Juventus.

Menaja anayehitajika ni yule ambaye atakuwa na uhakika wa kukibakisha kikosi hicho ndani ya nne bora kwenye Ligi ya England licha ya kutokuwa na ruhusa ya kufanya usajili.

Mourinho alishinda mataji mawili ya Premier League, matatu ya League Cup na FA Cup katika vipindi viwili ambavyo ameinoa timu hiyo.

Mara ya pili alifukuzwa kazi mwaka 2015 baada ya kuwa na msimu mbovu na siku zake za mwisho akiwa Chelsea alivurugana na aliyekuwa daktari wa kikosi hicho Eva Carneiro pia alizinguana na Eden Hazard ambaye kesho anaweza kutambulishwa rasmi Real Madrid.

SOMA NA HII  KOCHA HUYU ALIYEMNYOOSHA MBELGIJI WA YANGA ANAWINDWA ATUE JANGWANI