Home Habari za michezo KUELEKEA ‘SHOW’ YA JUMAPILI ….PHIRI AANDALIWA KUPELEKA ‘MAAFA’ JANGWANI…

KUELEKEA ‘SHOW’ YA JUMAPILI ….PHIRI AANDALIWA KUPELEKA ‘MAAFA’ JANGWANI…

Moses Phiri

Unaambiwa tayari Kocha Mkuu wa Simba raia wa Brazil, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, ameanza maandalizi ya kuiua Young Africans katika mchezo wa Debi ya Kariakoo kwa kumpa mbinu mpya Mshambuliaji wake raia wa Zambia, Moses Phiri.

Robertinho ambaye aliungana na Simba SC mapema mwaka huu akitokea Vipers Club ya Uganda, hadi sasa anasifika kutopoteza mchezo wowote tangu alipoanza kuifundisha klabu hiyo.

Chanzo chetu kutoka Simba SC kimeeleza kuwa, baada ya Phiri kuifunga Ihefu FC, Robertinho alikaa naye na kumpa mbinu atakazozitumia dhidi ya Young Africans, Jumapili (Novemba 05) mwaka huu.

“Kuna dalili za wazi hadi muda huu kuwa, Robertinho anamuandaa sana Phiri kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Young Africans, maana baada ya gemu yetu na Ihefu kumalizika tu, kocha alifanya kikao na Phiri na kumtaka ajiandae kwa ajili ya Young Africans jambo ambalo lilimfanya ampe mbinu nyingi,” kimeeleza chanzo hicho.

SOMA NA HII  KUHUSU KUMSAJILI ADEBAYOR...TRY AGAIN AENDELEA KUFUNGUKA ISHU ILIVYO...MUGALU HATARINI KUTEMWA...