Home Uncategorized Etienne kuiongoza Azam Fc msimu ujao

Etienne kuiongoza Azam Fc msimu ujao

Kama tulivyoripoti hapo awali kuhusu safari ya Etienne Ndayiragije kutoka KMC kwenda Azam Fc, hatimaye leo imetimia.

Kocha huyo aliyewahi kufanya vizuri na Vital’o ya Burundi, na pia kuiwezesha KMC kumaliza nafasi ya nne na kupata nafasi ya kucheza Shirikisho Adrika msimu ujao, amesaini Mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha klabu ya Azam Fc.

Hivyo, Etienne atakuwa na Azam katika michuano ya ndani na nje ya nchi msimu ujao.

The post Etienne kuiongoza Azam Fc msimu ujao appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  ABDI BANDA YUPO ZAKE BONGO, TIMU YAKE YAUZWA