Home Cecafa Cup YANGA KAZINI LEO KAGAME CUP, YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

YANGA KAZINI LEO KAGAME CUP, YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

 LEO Agosti Mosi timu ya Yanga itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Nyassa Big Bullets FC katika mchezo wa awali katika mashindano ya Kagame Cup.

Itakuwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 ambapo mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa.

Katika benchi la ufundi anatarajiwa kukaa kocha wa makipa Razack Siwa baada ya kocha mkuu Nasreddine Nabi kupewa mapumziko, pia kikosi nacho kina mabadiliko makubwa ambapo kitawatumia nyota wengi wa U 20.

Ni Ramadhan Kabwili huyu ni kipa mzawa kutoka timu ya wakubwa pia Juma Mahadhi ambaye alikuwa ndani ya Ihefu kwa mkopo amejumuishwa katika kikosi.

Pia ingizo jipya Dikson Ambundo kutoka Dodoma Jiji ni miongoni mwa nyota ambao wamejumuishwa katika kikosi. 

Kupitia ukurada rasmi wa Instagram wa Yanga umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao.

SOMA NA HII  KISA KUKOSEKANA KWA DIARA YANGA...MSHERY AWEKA REKODI HII YA KIBABBE CAF...MAMBO YAANZA KUWA MAZURI KWAKE...