Home Uncategorized MAJEMBE MAPYA YAWAPA JEURI AZAM FC,WATAMBA KUBEBA UBINGWA

MAJEMBE MAPYA YAWAPA JEURI AZAM FC,WATAMBA KUBEBA UBINGWA


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi mipango yao ya kugombania ubingwa msimu ujao mara baada ya kufanya usajili ambao unawapa jeuri kuelekea msimu mpya.

 

Azam katika msimu uliomalizika, ilijikuta ikimaliza ligi katika nafasi ya tatu huku ikishindwa kubeba taji lolote, jambo ambalo limesababisha uongozi wa timu hiyo kufanya usajili mkubwa.

 

 Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema kuwa imekuwa bahati mbaya kwa kumaliza msimu bila taji lolote, jambo ambalo limewachochea wafanye usajili ambao wanaamini utawapatia ubingwa msimu ujao.

 

“Azam ina falsafa ya kutwaa taji lolote katika kila msimu ila ilikuwa tofauti kwa msimu uliopita ambao haukuwa mzuri kabisa kwetu, jambo ambalo ilitubidi tuingie sokoni kwa ajili ya kujiimarisha.

 

“Ukiangalia usajili wetu, basi utagundua kuwa kuna kitu tunahitaji katika msimu ujao, nao ni ubingwa, tena ikiwezekana uwe ubingwa wa ligi kuu, hivyo sitarajii kuona kama tutashindwa kubeba ubingwa wowote kutokana na usajili mzuri tulioufanya,” amesema kiongozi huyo.


Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wamesajili na Klabu ya Azam FC ni Ally Niyonzima, Awesu Awesu, David Kisu.

SOMA NA HII  YANGA WAPEWA STRAIKA MGHANA, MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI