Home Habari za michezo MRITHI WA SENZO HUYU HAPA….YANGA WAAMCHOTA JUU KWA JUU KUTOKA KLABU...

MRITHI WA SENZO HUYU HAPA….YANGA WAAMCHOTA JUU KWA JUU KUTOKA KLABU KUBWA DR CONGO…JAMAA LINAJUA HILOO…


Yanga imempokea winga teleza, Tuisila Kisinda ‘TK Master’ aliyetua akitokea nchini Morocco alikokuwa akiichezea RS Berkane, lakini taarifa za kusisimua ni kwamba klabu hiyo inahesabu siku kabla ya kushusha Ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Zambia.

Tayari mabosi wa Jangwani wameanza mchakato wa kuzungumza na mtendaji huyo mpya kuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Senzo Mazingisa aliyeondoka mwishoni mwa mwezi Julai kurejea kwao Afrika Kusini.

Mabosi wa Yanga wanahitaji mtu atakayeanzia pale alipoishia Senzo aliyewahi kuwa CEO wa Simba na kufanya kazi na klabu kubwa za Afrika Kusini kabla ya kuja nchini na aliyehusika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko yaliyopo Jangwani kwa sasa.

Inaelezwa kuwa, CEO mpya atakayeingia kwenye rada za Yanga ni Mzambia anayefanya kazi katika moja ya klabu kubwa nchini DR Congo akiwa na rekodi tamu zilizowavutia mabosi wa Jangwani na kutaka kumleta nchini ili kuendeleza mambo mazuri yaliyoasisiwa na Msauzi aliyeondoka.

Hata hivyo, inaelezwa mchakato huo wa kuleta CEO mpya ili kuanza mipango ya Yanga kuingia kwenye mabadiliko ya kuendeshwa kwa mfumo wa hisa itakayotoa fursa kwa wawekezaji zaidi ya mmoja kumiliki 49% unafanywa kwa usiri mkubwa na vigogo wa timu hiyo.

“Vigogo wanaendelea na mipango yao, wakati tukimpokea Kisinda atakayeungana na timu kesho , pia kuna mchakato wa kuleta CEO kutoka DR Congo, ambaye ni raia wa Zambia, ila mambo yanafanywa kimyakimya ili kuwasapraizi wanachama na mashabiki, “ kilisema chanzo cha ndani.

Wakili Patrick Simon ndiye kwa sasa anayekaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa klabu tangu Senzo alipoachia ngazi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI