Home Uncategorized YANGA WAFICHUA SIRI YA KUITWANGA LIPULI TAIFA

YANGA WAFICHUA SIRI YA KUITWANGA LIPULI TAIFA


NAHODHA wa timu ya Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa walipewa mbinu na Kocha Mkuu Luc Eymael za kuwabana Lipuli jambo lililowapa ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Tshimbi amesema kuwa Eymael aliwaambia kwamba wanacheza na timu bora ni lazima wapambane kupata matokeo mapema jambo lililowapa nguvu ya kujiamini.

“Kocha alituambia kwamba tunacheza na timu bora na ngumu ni lazima tupambane kupata matokeo mapema jambo ambalo lilitupa matokeo haraka.

“Kipindi cha pili tulizidiwa mbinu ila tulilinda matokeo na tumefurahi kuondoka na pointi tatu muhimu,”.

Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi  34 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 17.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Mapinduzi Balama na Cernard Morrison wote walimaliza pasi za Juma Abdul huku lilel la Lipuli likifungwa na David Mwasa.

SOMA NA HII  NI SIMBA V NAMUNGO NUSU FAINALI, YANGA YAMSUBIRI MSHINDI WA LEO