Home Uncategorized KOCHA MANCHESTER UNITED: FERNANDES BADO HAJAFIKIA KUWA RONALDO

KOCHA MANCHESTER UNITED: FERNANDES BADO HAJAFIKIA KUWA RONALDO

OLE Gunnars Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa kiungo wake Bruno Fernandes hawezi kufananishwa na Cristiano Ronaldo kama wengi wanavyosema badala yake anacheza kama Paul Scholes.

Fernades amesajiliwa na Unted kwenye usajili wa mwezi Januari akitokea Klabu ya Lisbon kwa kitita cha pauni milioni 67.8 huku wengi wakimfananisha na Ronaldo.

“Ronaldo ni mchezaji wa tofauti na tunamamini kwamba Fernandes atakuwa na maisha mazuri ndani ya kikosi chetu na tutafanya naye mengi mazuri kwa ajili ya timu.

“Huyu ni mchezaji mzuri kwa kufunga lakini pia anaweza kutoa pasi za mabao kumfananisha na Ronaldo bado hajafikia hatua hiyo,” amesema.

SOMA NA HII  HAJI MANARA ATANGAZA KUSTAAFU, "NIPO SIMBA ILA NITAPUMZIKA KIDOGO "...