Home Yanga SC KAZE AKIRI PRESHA ILIKUWA KUBWA KWAKE

KAZE AKIRI PRESHA ILIKUWA KUBWA KWAKE


KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amekiri kuwa ni kweli ndani ya kipindi cha wiki moja iliyopita alikuwa katika mazingira magumu kutokana na presha ya matokeo mabaya ambayo kikosi chake kilikuwa kikipitia.

Kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka huu, Yanga juzi Jumamosi iliibuka na ushindi  kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam, hii ni baada ya kupata matokeo ya sare tatu mfululizo.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 49 baada ya kucheza michezo yao 21 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi.

Akizungumzia presha aliyokuwa akikumbana nayo Kaze amesema: “Tunashukuru kwa kupata ushindi kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Ni kweli ndani ya wiki moja iliyopita nimepata kujifunza vitu vingi kuhusu utamaduni wa soka la Tanzania, timu yetu haikuwa na matokeo mazuri na presha ilikuwa kubwa kwangu.

“Wachambuzi walikuwa wakitukosoa sana kiasi cha mashabiki wetu kupoteza imani, siwezi kubadilisha utamaduni huo lakini nikiri kuwa wiki moja iliyopita ilikuwa ngumu sana kwangu, lakini nimepata kujifunza mambo mengi pengine hata kuliko muda wote niliokuwepo Tanzania,”

SOMA NA HII  MANARA:- "SIMBA WAKIPATA HATA SARE...WACHINJE NGAMIA SABA...ATEMA CHECHE HIZI