Home news NAMUNGO KAMILI KUMALIZANA NA WAANGOLA LEO KIMATAIFA

NAMUNGO KAMILI KUMALIZANA NA WAANGOLA LEO KIMATAIFA


 KIKOSI cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco leo Februari 21 kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora dhidi ya 1 de Agosto, ya Angola.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Azam Complex na ule wa marudio pia utachezwa hapo kwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) liliamua iwe hivyo.

Awali mchezo wa kwanza ulipaswa kuchezwa Februari 14, nchini Angola ila wachezaji wa Namungo FC ambao ni watatu pamoja na kiongozi mmoja mamlaka  ya Angola ilieeleza kuwa wamekutwa na Virusi vya Corona hivyo waliamuru timu nzima ikae karantini.

Jambo hilo lilipingwa na viongozi pamoja na timu kiujumla mpaka pale Caf ilipoamua kuufuta mchezo huo kisha ikaamua kwamba mechi zote zichezwa Dar kwa kuwa uchunguzi wao umegundua kwamba hakukuwa na timu iliyokuwa na mpango wa kupanga matokeo.

Morroco ambaye kwenye safu ya ushambuliaji anamuamini Stephen Sey huku Bigirimana Blaise ambaye naye ni mtambo wa mabao atakosekana kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha amesema kuwa watapambana kupata matokeo.

“Makosa ya mechi zilizopita tumefanyia kazi hivyo kwenye mchezo wetu wa kwanza hatua hii ya 32 bora tutapambana kupata matokeo chanya.

“Mashabiki wajitokeze kutupa sapoti tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

Mchezo wa leo ambao Namungo ni wageni utachezwa majira ya saa 11:00 jioni utagharamiwa na Waangola huku ule wa marudio ukitarajiwa kuchezwa Februari 25.

SOMA NA HII  MWAKINYO AZIDI KUPOROMOKA KIMATAIFA...HAYUPO TENA HATA KUMI BORA...