Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUMTUPIA VIRAGO VYAKE JANGWANI….MOLOKO ‘AOKOTWA’ NA WAARABU…

BAADA YA YANGA KUMTUPIA VIRAGO VYAKE JANGWANI….MOLOKO ‘AOKOTWA’ NA WAARABU…

Habari za Yanga leo

Aliyekuwa winga wa Yanga, Jesus Moloko ambaye alikuwa akihusishwa na Geita Gold dirisha dogo la usajili lililopita, amejiunga Al Sadaqa SC Benghazi inayoshiriki Ligi Kuu ya Libya.

Moloko alitemwa na Yanga kupisha usajili wa winga Mghana Augustine Okrah aliyetua klabuni hapo akitokea Bechem United ya nchini kwao.

Geita ilipambana ili kumpata Moloko katika dirisha dogo la usajili na mazungumzo hayakuzaa matunda na sasa atakipiga ligi moja na aliyekuwa mshambuliji wa mshambuliaji wa Simba Jean Baleke.

Baleke amesajiliwa ya Al Ittihad baada ya TP Mazembe kumtoa tena kwa mkopo na alimalizana na Simba baada ya muda wake wa mkopo kumalizika sasa atakuwa akikiwasha katika klabu hiyo, hadi Januari 30, 2025.

Timu hiyo ambayo kwenye msimamo wa ligi ya Libya iko nafasi ya nane baada ya kucheza michezo tisa na ina pointi 6 imeandika kwenye mitandao yake ya kijamii taarifa inayosema “Muda mchache kabla ya dirisha la usajili kufungwa winga Mkongomani Jesus Moloko atakuwa sehemu ya ngome yetu akitoka Yanga ya Tanzania”

SOMA NA HII  WAKATI ZAIDI YA MAKOCHA 80 WAKIOMBA KAZI...KOCHA MPYA SIMBA NI HUYU HAPA...UONGOZI WATOA TAMKO RASMI...