Home Habari za michezo WAMEAMUA….KILA GOLI MOJA KWA SIMBA NI MIL 1.5,….WASHINDWE WENYEWE TU…..

WAMEAMUA….KILA GOLI MOJA KWA SIMBA NI MIL 1.5,….WASHINDWE WENYEWE TU…..

FT:Simba 1-0 Jamhuri

PAMOJA na kukiri kuzidiwa na Simba, Tembo FC imesema inahitaji rekodi ya kuwafunga wapinzani wao hao bila kujali matokeo ya jumla ili kuandika historia, huku mabosi wakitangaza dau la Sh1.5 milioni kwa kila bao litakalopatikana kuhakikisha Mnyama anakufa mapema.

Tembo ya mkoani Tabora inatarajia kushuka uwanjani kesho, Jumatano kuumana na Simba katika mchezo wa kiporo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.

Katibu Mipango wa timu hiyo, Iddrisa Yusuph amesema uongozi katika kuamsha morali na mzuka kwa wachezaji wametenga Sh1.5 milioni kwa kila bao bila kujali matokeo ya jumla ili kuandika historia ya kuifunga Simba.

“Sisi ni Tembo, wao ni Simba ina maana wanyama wakali msituni tunakutana. Uongozi umeweka mipango mizuri na kuonyesha tunaitaka hiyo mechi tutanunua kila bao Sh1.5 milioni. Tumewaambia wachezaji wapambane tuweke historia,” amesema Yusuph.

Timu hiyo kongwe ambayo haishiriki ligi yoyote iliyoanzishwa 1987 ikiwa chini Halmashauri ya Nzega kabla ya kurejeshwa kwa wananchi, inakutana na Wekundu wa Msimbazi kwa mara ya kwanza katika historia mchezo ambao utapigwa jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ramadhan Kilobi amesema wanafahamu Simba ni timu kubwa ndani na nje ya uwanja, lakini hawataingia kinyonge badala yake watapambana kutafuta matokeo mazuri.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa katika maandalizi mazuri ikiwamo mechi za kirafiki dhidi ya Tabora United ya Ligi Kuu waliyocheza nayo majuzi na kufungwa mabao 3-1 na kwamba, vijana wake wapo tayari kuikabili Simba.

“Mchezo utakuwa mgumu. Tunajua kabisa Simba wametuzidi kila kitu na tupo tayari kwa matokeo yoyote, ila tunataka kuwafunga ili tupate cha kusimulia. Kuna wachezaji kama Willy Onana na Fabrice Ngoma lazima tukomae nao,” amesema Kilobi.

Nahodha wa timu hiyo, Rajabu Twaha amesema wapo fiti kisaikolojia na matarajio ni kuipambania Tembo FC kuhakikisha wanaandika historia dhidi ya vigogo wa soka nchini na watakuwa makini kwa mchezaji mmoja mmoja kutofanya makosa.

“Tunaijua Simba na tumeifuatilia kwa muda mrefu. Tutajua wapi tuwashike kadri mchezo utakavyokuwa. Tumejiandaa kisaikolojia na tutamchunga yeyote kwa sababu wapinzani (wetu) wana kikosi kipana,” amesema nyota huyo mkongwe kikosini hapo.

KIBOKO YA SIMBA
Itakumbukwa kwamba, Desemba 26, 2018 Simba iliondolewa katika mashindano hayo na Mashujaa FC ya Kigoma wakati huo ikiwa katika Ligi Daraja la Kwanza Bara. Timu hiyo kwa sasa imepanda Ligi Kuu Bara, lakini bado haijakutana na Mnyama katika mchezo wowote tangu ipande.

Siyo Mashujaa tu, lakini msimu mmoja nyuma Simba iling’olewa katika michuano hiyo na Green Warriors ya Tabora kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

SOMA NA HII  'ABRAKADRA ' ZA MAYELE NA YANGA KWISHNEII...UKWELI KUHUSU DILI LAKE NA WAARABU HUU HAPA...