Home kimataifa KAKA ANA TUZO KIBAO KABATINI MWAKE

KAKA ANA TUZO KIBAO KABATINI MWAKE


 AMELETWA duniani Aprili 22,1982 ana umri wa miaka 39 ni raia wa Brazil jina lake anaitwa Ricardo Izecson dos Santos Leite ila jamii inamjua kwa jina la Kaka.

Amecheza jumla ya mechi 529 amefunga mabao 161 na pasi 147 ni kwa mechi za ushindani ndani ya ligi pamoja na mashindano mengine ni miongoni mwa wachezaji wenye tuzo kibao kabatini.

Ni Serie A huko rekodi zinaonyesha amecheza mechi nyingi ambazo ni 223 na alitupia jumla ya mabao 77 na pasi 63. Alicheza ndani ya Real Madrid msimu wa 2009/2013 alitokea AC Milan alipodumu kuanzia msimu wa 2003/09 na alirejea tena katika timu hiyo msimu wa 2013/14.

SOMA PIAJACK GREALISH KUIBUKIA MANCHESTER CITY

Nafasi yake anayocheza ni kiungo mshambuliaji ni miongoni mwa wachezaji nane duniani ambao wameweza kushinda Taji la Kombe la Dunia ilikuwa 2002, UEFA Champions League pamoja na Ballon d’Or ilikuwa ni msimu wa 2007.

Pia ana tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa FIFA ilikuwa ni 2007 alipokuwa AC Milan ikiwa ni mafanikio makubwa kwa nyota huyo ambaye alistaafu soka mwaka 2017 alipokuwa na timu ya Orlando City SC.

Akiwa na timu ya taifa ya Brazil ameweza kushiriki Kombe la Dunia mara tatu ilikuwa ni 2010,2006 na 2002.

Msimu wa 2006/07 alikuwa mfungaji bora katika UEFA Champions League alipotupia jumla ya mabao 10 alikuwa ndani ya AC Milan.

SOMA NA HII  TETESI ZA USAJILI: MESSI KUNG'OLEWA PSG...WAARABU WAMPA MIL 1 KILA DK 1...POGBA ACHEZA DK 35 MSIMU MZIMA