Home Azam FC AZAM FC BADO IPO CHIMBO KUSHUSHA MAJEMBE YA KAZI

AZAM FC BADO IPO CHIMBO KUSHUSHA MAJEMBE YA KAZI


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kwamba bado upo chimbo kwa sasa kuendelea kusaka majembe mapya kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Tayari Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwanamina imemalizana na majembe saba ya kazi ikiwa ni pamoja na Wazambia, watatu ambao ni  Charles Zulu, Paul Katema na Rodgers Kola, Mkenya Kenneth Muguna na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama pamoja na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo.

Pia yupo kipa Ahmed Ali Suleiman ambaye ni mzawa alikuwa akikipiga ndani ya kikosi cha KMKM ya Zanzibar.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin alisema kuwa kazi kubwa iliyopo kwenye kikosi hicho ni kujenga wingo mpana kwa ajili ya mashindano ya kimataifa pamoja na ligi.

“Hatujamaliza bado kazi inaendelea hivyo licha ya kwamba tumesajili ikitokea mwalimu akatuambia kuna jambo tunapaswa kufanya basi itakuwa hivyo.

“Tunashiriki kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao na tuna kazi ya kushiriki kwenye ligi hivyo ni lazima tujipange kuwa imara kwa ajili ya ushindani,” alisema Amin.


SOMA NA HII  ZA CHINI CHINI....AZAM FC NAO 'WAAMUA KUFAGIA JALALA'....WAPANGA KUTEMA MASTAA WAO WOTE...AJIBU, MBOMBO BYE BYE...