Home Simba SC SIMBA WAZIDIWA AKILI NA YANGA, KWA STAA HUYU WA KONGO

SIMBA WAZIDIWA AKILI NA YANGA, KWA STAA HUYU WA KONGO

Achana na tripu ya Malawi ambayo wanaenda Wachezaji mseto, Yanga inachanga karata zake wa mwisho kukamilisha usajili wake kabla ya kuingia rasmi kambini wiki ijayo.

Lakini wameshtukia jambo. Wamepokea simu kutoka DR Congo kwamba kuna wazito wa Simba wameweka mzigo mezani wanataka kumaliza dili la yule winga Maxi Nzengeli ambaye anaichezea Maniema. Siyo huyo tu hata yule jezi namba 6 wa Asec ambaye Yanga wanamtaka Simba wamemvutia waya.

Simba ambayo inakusanyana Dar es Salaam tayari kwa safari ya kambini Uturuki, baada ya kupata faili la winga huyo wakatua kama mwewe na kuanza kupiga hesabu za kuwatibulia watani wao katika dili hilo ambapo nao wakamuwekea mzigo mrefu mezani.

Wekundu hao ambao usajili wao ni kama umeshakamilika kwa asilimia kubwa wameiwekea dola 150,000 (sh361 milioni), klabu yake ya Union Maniema ili wanunue mkataba wake wa miaka miwili uliosalia wamchukue fasta kuwatia adabu Yanga ambako wamekuwa wakiringia uswahiba wao na Wakongo hao.

Fedha hizo zimewashtua mabosi wa Maniema ambapo wanajadili mezani kama wabaki kuheshimu mahusiano yao na Yanga au wachukue fedha kuendelea na maisha wakisubiri jibu la bosi wao wa juu wa klabu ambaye ni mtu mzito katika jeshi la nchi hiyo.

“Unajua jenerali ana uhusiano mkubwa na watu wa Yanga ila hii ni biashara ingawa bado timu zote hakuna iliyomaliza kulipa chochote,” alisema bosi huyo wa Maniema.

“Mchezaji bado ana mkataba wa miaka miwili na hakuna ambaye atapata mchezaji bila kumalizana na klabu, tutajua baadaye wiki hii nani atafanikiwa kati ya Yanga ambao walitangulia au Simba ambao wamekuja baadae,”aliongeza ingawa Mwanaspoti linajua Simba imeambiwa na Enock Inonga kwamba jamaa anajua. Ni mtu.

SOMA NA HII  TIZI LA YANGA SIO POA KAMA ULAYA UNAAMBIWA