Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI vs AL AHLY….ONANA AKUMBUSHIA ALIVYOWAFANYA WYDAD KWA MKAPA….

KUELEKEA MECHI vs AL AHLY….ONANA AKUMBUSHIA ALIVYOWAFANYA WYDAD KWA MKAPA….

Habari za Simba leo

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Cameroon na Simba SC, Willy Onana, amesema huu ndiyo wakati muhimu kwa timu yake kwenda kuandika historia mpya Barani Afrika kwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Simba SC wapo katika maandalizi ya kuwavaa mabingwa wa Misri, Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, mchezo utakaochezwa ljumaa (Machi 29) saa 3.00 usiku, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Akizungumza walipokuwa visiwani Zanzibar ambapo timu yake imeweka kambi, Onana amesema anajua wanaenda kupambana na bingwa mtetezi, hivyo hautakuwa mchezo rahisi kwao lakini ndiyo wakati wa kuonyesha ubora wao kwa kutimiza malengo yao ya muda mrefu.

“Binafsi najisikia vizuri kucheza Robo Fainali kwa mara ya kwanza, Al Ahly ni kama Real Madrid kwa Afrika inaweza kuwa katika kipindi cha mpito lakini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wanakuja kivingine.

Tunatambua tunakwenda kucheza na timu kubwa sana barani Afrika, hizi ni nyakati bora kwa wachezaji na viongozi wa Benchi la Ufundi kuandika historia mpya,” amesema Onana.

Amesema kama kuna aliyekuwa akiingalia Simba SC ikiishia hatua ya Robo Fainali abadilishe mtazamo kwa kuwa huu ni wakati wa kwenda kubadili hii historia ambayo kwa muda mrefu wamekuwa wakiisubiri.

“Sijui mipango ya mwalimu katika mchezo huo lakini mimi binafsi niko tayari kwa ajili ya mechi hii kubwa ambayo itatazamwa na watu wengi Barani Afrika,” amesema Onana.

Simba SC imefika hatua hiyo baada ya kuishia nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi B kwa alama tisa nyuma ya Asec Mimosas ya Ivory Coast ikiwa na alama 12.

SOMA NA HII  MASAU BWIRE AFUNGUKA NAMNA ALIVYOPEWA OFA SIMBA, AMTAJA MANARA