Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO….KMC FC NAO WAONA ISIWE TABU…WAIBUKA NA KUSAJILI KIFAA HIKI...

KUELEKEA MSIMU UJAO….KMC FC NAO WAONA ISIWE TABU…WAIBUKA NA KUSAJILI KIFAA HIKI HATARI KUTOKA AZAM FC…

Kiungo Mshambuliaji wa Azam FC, Awesu Awesu amejiunga na klabu ya KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Azam Awesu sasa amesajiliwa rasmi na klabu ya KMC ambayo aliitumikia kwa mkopo na kufanikiwa kuonesha kiwango kikubwa kwenye kikosi hicho.

Awesu ambaye alisajiliwa na klabu ya Azam akitokea klabu ya Mtibwa Sugar, wakati akiwa kwenye kikosi cha Azam FC kiungo huyo hakufanikiwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa chini ya kocha Lwandamina na kupelekwa kwa mkopo kwenye kikosi cha KMC.

Akizungumzia usajili huo, Awesu amesema kuwa;

“Mkataba wangu na Azam umemalizika lakini tayari nimesaini mkataba wa mwaka mmoja na KMC.

“Ni changamoto mpya kwangu lakini hiyo hainipi shida kwani nimecheza kwa msimu uliopita hivyo nitaendelea kupambana.”

SOMA NA HII  KUHUSU KUFANYA KAZI NA MGUNDA....MBRAZILI SIMBA 'ACHOCHEA UKUNI JIKONI'...