Home Habari za michezo SHAFII DAUDA AIBUKA NA HAYA SAKATA LA MANARA KUFUNGIWA NA TFF…AWASHUKIA WANAOMTETEA...

SHAFII DAUDA AIBUKA NA HAYA SAKATA LA MANARA KUFUNGIWA NA TFF…AWASHUKIA WANAOMTETEA KISA UYANGA WAKE…


Ikiwa zimepita siku mbili tu tangu kufungiwa kwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara kujihusisha na Soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili.

Wadau wa Soka wamegawanyika juu ya hukumu hiyo, kuna wanaosapoti na kuna wale wanaoona Msemaji huyo ameonewa.

Sasa Shaffih Dauda ni Mwandishi wa Habari na mchambuzi wa michezo ambae nae yupo ndani ya kifungo cha Soka kwa muda wa miaka mitano, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

“Kuna vitu havipo sawa kwenye mpira kisa Usimba na Uyanga, kuna muda tunataka kubadili nyeupe kuwa nyeusi kisa Usimba na Uyanga, this is not fair.

Nalitazama sakata la Haji Manara na hukumu ya miaka miwili namna watu wengi wanavyopinga hukumu na kuipa presha kubwa sana TFF, hiyo haipo sawa.

Mlikuwa wapi wakati Mbwana Makata anapigwa miaka mitano, Lwitiko wa Mbeya anachukua miaka 10, kuna yule Kiongozi wa Biashara United kafungiwa maisha na hata Mimi nimepigwa miaka mitano.

Haji sio exceptional ni Mwanafamilia ya mpira kama ilivyo kwa wengine, anapopewa hukumu kwa mujibu wa kanuni haipaswi kuonekana ameonewa, kumbuka hata Mimi nilifungiwa kisa tu MAKALA tena ya mtandaoni, why not Haji dhidi ya Rais wa TFF?

Tunaupa taswira gani mpira wetu? Tunamaanisha kosa likifanywa na vigogo wa Kariakoo it means linapaswa kufumbiwa macho? Jibu ni HAPANA, binafsi ni muumini wa utawala wa sheria.

Kila kitu kipo wazi sana, kama Haji hajaridhishwa na hukumu anapaswa kukata rufaa, ni haki yake! Sioni mantiki ya press na kusigana bila sababu, ni kuonesha mnataka kuwa juu ya mfumo.

Sioni sababu ya mvutano, Haji na Yanga wana vitu viwili tu vya kufanya kwasasa, kukata rufaa kama hawajaridhika au kukaa kimya ili Haji atumikie adhabu yake, nje na hapo ni kuunajisi mpira wa miguu na kupoteza sifa nzuri tunayoanza kuijenga

Nawaelewa nyote kuwa mnaamini kwenye haki na sheria, lakini kuna utaratibu wake, napenda sana kumuona Ndugu yangu Haji kwenye mpira ila kuna utaratibu wake nae anafahamu, basi muufuate

SOMA NA HII  FT: YANGA SC 4-0 MBEYA KWANZA...HATIMAYE MAYELE KAONA MWEZI...BADO POINTI SITA TU KISHINDO KILIE JANGWANI...

Tunapocodify na kuweka mifumo ituongoze ni kwakuwa tunafahamu sie ni Binadamu na huwa tunakosea, hatuwezi kwenda bila mfumo na sio kwa ubaya, inapokuja sheria haipaswi kuwa Simba wala Yanga bali sheria”