Home Uncategorized SIMBA WAREJEA BONGO KUIWAHI AZAM FC

SIMBA WAREJEA BONGO KUIWAHI AZAM FC


KIKOSI cha Simba baada ya kumaliza mchezo wao wa kimataifa dhidi ya UD do Songo nchini Msumbiji kilikwea pipa na kurejea Bongo.

Simba walikuwa ugenini, karata yao ya kwanza kimataifa hatua ya awali wamelazimisha suluhu kwani mpaka dakika 90 ubao ulikuwa unasoma 0 kwa UD do Songo pamoja na Simba.

Mchezo wa marudio kimataifa unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 jijini Dar.


Kikosi kimerejea mapema kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC utakaochezwa Agosti 17 Uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  YANGA: TUPO TAYARI KUIVAA MWADUI FC, WAMSHUKURU MUNGU KUWALINDA