Home Uncategorized NAMUNGO YAANZA KUIVURUGA BIASHARA UNITED

NAMUNGO YAANZA KUIVURUGA BIASHARA UNITED

MLINDA Mlango namba moja wa kikosi cha Biashara United, Nurdine Barola raia wa Burkina Faso anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Namungo FC ambacho msimu ujao kitashiriki Ligi Kuu Bara.

Barola alikuja bongo kwa lengo la kujiunga na Yanga dili lake likatibuka na kudondokea mikononi mwa mabosi wa Biashara United ya Mara ambayo imebaki ligi kuu msimu ujao.

Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa mipango ya usajili ipo kwa ajili ya kuboresha kikosi hivyo mambo yakiwa sawa kila kitu kitakuwa wazi.

Endapo dili lake litatimia atajiunga na kocha wake wa zamani wa Biashara United ambaye kwa sasa anakinoa kikosi hicho, Hitimana Thiery.

SOMA NA HII  BABAYE KAGERE NI MTANZANIA, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI