Home Uncategorized UKIACHANA NA WALE WANAOTEMWA YANGA, HAWA HAPA WANATOLEWA KWA MKOPO

UKIACHANA NA WALE WANAOTEMWA YANGA, HAWA HAPA WANATOLEWA KWA MKOPO


Wakati maboresho ya kikosi cha Yanga yakiendelea kufanyika hivi sasa kwa kusajili wachezaji wapya, baadhi wametajwa kuondolewa kwa mkopo.

Yanga hivi sasa imesajili wachezaji takribani saba wapya ikiwa na malengo makubwa ya kuurejesha ubingwa wake baada ya kuukosa kwa misimu miwili mfululizo.

Wachezaji wanaotajwa kuondolewa kwa mkopo ni pamoja na Mrisho Ngasa, Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Wengine ni Deus Kaseke, Jaffar Mohamed na Mohamed Issa Banka.

Kumekuwa na tetesi hizi japo bado uongozi haujataka kuliweka wazi kinagaubaga juu ya wapi wataelekea na itakuwa lini.

SOMA NA HII  LIPULI YASAJILI MAJEMBE NANE YA KAZI, DIDA WA SIMBA NA YANGA NDANI