Home Uncategorized LIPULI: HATUNA MKWANJA ILA KOMBE TUNASEPA NALO

LIPULI: HATUNA MKWANJA ILA KOMBE TUNASEPA NALO

KOCHA wa timu ya Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa bado hali ndani ya kikosi kwa upande wa uchumi haijakaa sawa ila amewajenga kisaikolojia wachezaji wake kubeba kombe la FA mbele ya Azam FC Juni Mosi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa tatizo la ukata limekuwa sugu ukichanganya na ugumu wa ratiba kwake ila hilo ameweka pembeni na kulipigia hesabu kombe.

“Kwa sasa kikosi kina hali mbaya kiuchumi najua kabisa sina hela ila nimewajenga wachezaji wangu kupambana na tutapata matokeo kwenye mchezo wetu uwanja wa Ilulu.

“Ushindani ni mkubwa na timu ninayocheza nayo ipo vizuri kwenye kila idara ila hilo halinipi taabu, nimezungumza kuhusu kubwana na ratiba sasa ninakwenda kuonyesha kazi yenyewe uwanjani mpaka nibebe kombe,” amesema Matola.

SOMA NA HII  NI SALAAAM, FALCAO AWEKA REKODI MWANZA YANGA IKIENDA SARE YA 1-1 NA PAMBA