Home Uncategorized AZAM FC: TUPO TAYARI KUWA WA KIMATAIFA

AZAM FC: TUPO TAYARI KUWA WA KIMATAIFA

KOCHA wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Lipuli Juni Mosi uwanja wa Ilulu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa hana mashaka na ubora wa kikosi chake hivyo ushindi ni suala la muda tu.

“Tupo imara kiushindani na kikosi chetu tunakipanga kutokana na mahitaji ya fainali yenyewe inataka nini, kila mmoja ana morali ya kupambana kwa ajili ya timu.

“Mchezo utakuwa mgumu, ila tumejipanga kukabiliana na ugumu huo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema Cheche. 

Bingwa wa kombe hilo anaipeperusha Bendera ya Taifa kwenye michuano ya kimataifa.
SOMA NA HII  MOROCCO KUMSAKA MBADALA WA ADAM SALAMBA