Home Habari za michezo ZA NDAANI KABISAA….SIMBA WAMALIZANA NA BEKI WA IHEFU….TSHABALALA AJIANDAE PA KWENDA…

ZA NDAANI KABISAA….SIMBA WAMALIZANA NA BEKI WA IHEFU….TSHABALALA AJIANDAE PA KWENDA…

Habari za Usajili Simba SC

Usiku wa kuamkia jana ‘Jumanne’ kabla ya kuanza safari ya kurudi Dar Mabosi wa Simba wamemalizana na beki wa kushoto wa Ihefu, Yahya Mbegu na tayari amemwaga wino kwa mkataba wa miaka miwili.

Mbegu anakwenda kuwa mbadala sahihi wa Mohammed Hussein ambae kwa muda mrefu ametawala eneo hilo.

Kwa takribani zaidi ya misimu mitano sasa, Mohamed Hussein amekuwa akitumika mara kwa mara huku Gardiel Michael akishindwa kufua dafu mbele yake.

Hata hivyo, inatajwa kuwa Tshabalala anatakiwa na timu moja kubwa ya Afrika kusini, hivyo pengine Simba wameona wapate mbadala sahihi wa kuweza kushika nafasi hiyo.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA SC KINACHOANZA DHIDI YA ASEC MIMOSA