Home Habari za michezo HII HAPA TIMU YA AFRIKA WANAOTAKA KUMPA AJIRA YA UKOCHA MOURINHO….

HII HAPA TIMU YA AFRIKA WANAOTAKA KUMPA AJIRA YA UKOCHA MOURINHO….

Habari za Michezo

Majadiliano kati ya Kocha kutoka nchini Ureno Jose Mourinho na Shirikisho la Soka nchini Cameroon ‘FECAFOOT’ yanaonekana kupiga hatua kubwa kwa ajili ya kocha huyo kuinoa ‘The Indomitable Lion’.

Cameroon imekuwa katika mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu wa Mpya wa Kikosi chao cha Taifa, baada ya kuachana na Kocha mzawa Rigobert Song mwezi uliopita.

José Mourinho anatafuta changamoto mpya baada ya kuachana na klabu ya AS Roma ya Italia Januari 2024, kufuatia mfululizo mbaya wa matokeo ligi kuu Italia.

‘The Special One’ anaweza kuchukua mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya Cameroon endapo mazungumzo yatakwenda vizuri na Cameroon.

Ingawa Mourinho anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa mshahara unaweza kuwa kikwazo kati yake na Cameroon.

SOMA NA HII  RASMI...AZAM FC WANYOOSHA MIKONO JUU UBINGWA WA LIGI KUU...WAFUNGUKA SABABU YA NDOTO KUYEYUKA...