Home Simba SC KOCHA WA WAARANU WA MISRI AWAPIGA MKWARA SIMBA

KOCHA WA WAARANU WA MISRI AWAPIGA MKWARA SIMBA


PITSO Mosimane, Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri amesema kuwa kipigo chao cha bao 1-0 ambacho walikipata mbele ya Simba wamekifanyia kazi hivyo wataingia Uwanja wa Mkapa kwa tahadhari.

Al Ahly msimu wa 2018 ilipokuja Bongo Februari 2019 ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa hatua ya makundi.

Bao pekee la ushindi kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes lilipachikwa kimiani na Meddie Kagere ambaye bado yupo na kikosi hicho ambacho kinatarajiwa kumenyana na Waarabu hao wa Misri.

 Kocha huyo ambaye aliwahi kufanya kazi na kiungo  wa Simba, Luis Miqiussone 2018 alipokuwa ndani ya Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ila alimtoa kwa mkopo kwa kile ambacho aliweka wazi kuwa kijana huyo kiwango ilikuwa bado sana.

Tayari Kikosi cha wachezaji 22 wa Al Ahly ya Misri wapo ndani ya Bongo walitua Februari 19, 2021 usiku kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.

Kocha huyo amesema:”ipo wazi kwamba waliwahi kutufunga Uwanja wa Mkapa lakini yale makosa tumeyafanyia kazi hivyo tutaingia ndani ya uwanja kwa juhudi za kusaka ushindi.

“Kila kitu kipo sawa na maandalizi yapo vizuri kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi ndani ya uwanja,”.


SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA WAISAGIA KUNGUNI YANGA, UWANJA WA AZAM COMPLEX KISA USHINDI, ISHU IKO HIVI