Home Yanga SC MWALIMU KASHASHA:CARLINHOS ANA UWEZO BINAFSI,MTIBWA WALIZIDIWA KIDOGO

MWALIMU KASHASHA:CARLINHOS ANA UWEZO BINAFSI,MTIBWA WALIZIDIWA KIDOGO


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Bongo, Alex Kashasha, maarufu kwa jina la Mwalimu Kashasha amesema kuwa wachezaji wa Yanga waliamua matokeo kwa mabadiliko ya kiufundi na kimbinu yaliyofanywa na mwalimu Cedric Kaze.


Yanga ilishinda bao 1-0 lilipachikwa na Carlos Carlinhos, raia wa Angola ambaye alitokea benchi na kubadili matokeo ndani ya dakika mbili ambazo alizitumia.

Kashasha amesema kuwa uwezo binafsi wa wachezaji wa Yanga ikiwa ni pamoja na Muangala huyo jambo ambalo liliwafanya Mtibwa Sugar wasiwe na chaguo ndani ya Uwanja wa Mkapa kwa kuwa walizidiwa kidogo.

“Ukitazama mchezo kiujumla timu zote zilikuwa zinacheza mfumo mmoja, sasa Yanga wao waliamua kuwazidi kwenye upande wa spidi jambo ambalo liliwatesa wapinzani wao.

“Kwa upande wa Mtibwa Sugar mbinu zao zilikuwa bora na imara ila walikuwa na mshambuliaji mmoja mbele jambo ambao liliwapa wakati mgumu kuweza kupata matokeo.

“Ukweli ni kwamba ligi ya Tanzania wengi wanafikiria ni nyepesi ila ni ngumu na ina ushindani mkubwa kikubwa ni kila mmoja kupambana kufikia malengo ambayo amejiwekea,” amesema.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 49 kibindoni baada ya kucheza mechi 21 huku Mtibwa Sugar ikiwa imebaki na pointi zake 23.
SOMA NA HII  BAADA YA KIWANGO 'KUNTU'...'FEI TOTO' APELEKWA KUCHEZA SOKA LA KULIPA NNJE YA NCHI..