Home news KUHUSU ISHU YAKE YA KUJA YANGA…CHIKO USHINDI AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z MCHONGO ULIVYO….

KUHUSU ISHU YAKE YA KUJA YANGA…CHIKO USHINDI AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z MCHONGO ULIVYO….


MASTAA wa Yanga wanaendelea kupigishwa tizi la nguvu kambini wakijiandaa kuvaana na Biashara United leo Jumapili, lakini huku nyuma kiungo mshambuliaji wa TP Mazembe, Chico Ushindi amefunguka kuwa anakuja Jangwani kuwasha moto.

Yanga inapambana kumbeba Ushindi anayetumia miguu yote miwili ili kuziba nafasi ya Yacouba Songne aliye majeruhi, likiwa ni chaguo la Kocha Nasreddine Nabi anayetaka mtu anayeweza kucheza wingi ya kushoto ambayo bado haijampata mtu sahihi licha ya Farid Mussa kuwepo.

Nyota huyo, amefunguka juu ya dili lake hilo na Yanga na kusema kuwa ameshafanya mazungumzo ya awali tu na Yanga na kama mambo yataenda sawa atakuja kukinukisha kwani amekuwa akihamasishwa na uwepo wa Wakongomani wenzake kikosini.

Ushindi mwenye umri wa miaka 25 ameweka wazi dili lake linakwama kumalizwa mapema kwa vile bado ana mkataba Mazembe na anachosubiri kwa sasa ni mabosi wake kumalizana na wale wa Yanga aje kucheza kwani amevutiwa mno kujiunga na vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

“Mimi nilisaini mkataba wa miaka mitano na nimecheza miaka mitatu hadi sasa, hivyo bado miaka miwili mbele, hapo Mazembe wanakaa na Yanga kuzungumza,” alisema Ushindi na kuongeza kuwa, upande wake yupo tayari kuja kucheza Yanga na kuisaidia timu hiyo kuchukua makombe mbalimbali.

“Niko tayari kuja Yanga muda wowote kuanzia sasa, lakini nasubiri niambiwe kama viongozi wa timu hizo mbili wanamalizana,” alisema Ushindi na kuongeza;

“Desemba 29 nitakuwa Lubumbashi nadhani nitajua kila kitu kutoka upande wa Mazembe kuhusu Yanga.”

Ushindi anasifika kwa ubora mkubwa wa kucheza nafasi za wingi zote, pia kucheza kama straika na namba 10 uwanjani na hilo ndilo linalowapa mzuka mabosi wa Yanga kupambana kwa kila namna hata kumchukua mchezaji huyu kwa mkopo kama watashindwa kuvunja mkataba wake.

MAYELE NA BANGALA

Licha ya mabosi wa Yanga kupambana kumbeba Ushindi, lakini nyuma ya mzuka wake ni mastaa watatu wa Jangwani wanaotaka atue kuungana naye.

Ushindi alisema amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na Yannick Bangala, Fiston Mayele na Djuma Shabani na wanamsisitizia asichomoe katika dili hilo la kuja Yanga.

SOMA NA HII  AFISA HABARI MPYA SIMBA AVUNJA UKIMYA KUHUSU MAHABA YAKE KWA YANGA...ADAI NI KWA MIAKA KUMI .....

“Uwepo wa Bangala na Djuma katika kikosi cha Yanga kimenifanya niridhike kuwa, kikosi cha timu hiyo kinaundwa na mastaa wanaotaka mafanikio.”

Winga huyo alisema mastaa hao wamemwambia kuwa Yanga kuna maisha matamu chini ya wadhamini wao GSM pamoja na vibe la mashabiki wa timu hiyo.

“Naongea sana na Djuma na Bangala hawa ni rafiki zangu sana wameniambia Yanga wakinifuata tu nipambane kuhakikisha nakuja huko, wanasema Yanga ina timu nzuri na sasa wanaongoza ligi na watachukua ubingwa, nimefurahi kusikia hivyo,” alisema Ushindi.

“Wananiambia pia kuna wadhamini wao GSM wanalipa vizuri hakuna matatizo yoyote, wamenitumia na video wananiambia hata mashabiki wa Yanga wanawapenda sana nyota wao na timu yao. Hizi ni taarifa nzuri sana ambazo mtu yeyote angependa kucheza hapo,” alisema.

Ushindi pia aliongeza anatamani kucheza sambamba na mshambulaiji Fiston Mayele ambaye alikuw akikutana naye wakiwa timu tofauti.

“Mayele namjua ni mshambuliaji mzuri hapa Congo ningependa sasa kucheza naye timu moja, tulikuwa tunakutana timu za taifa na wakati mwingine akiwa na klabu yake ya AS Vita mimi nikiwa hapa Mazembe,” alisema Ushindi na kuongeza;

“Nimewaambia viongozi wa klabu (Mazembe) nataka kuondoka na ikija Yanga wanifanyie mambo rahisi niondoke hapa, najua wataweka ngumu mimi kuniuza, lakini niko tayari hata kutoka kwa mkopo kwanza nije hapo Yanga.”

NABI NA TIZI

Wakati hali ikiwa hivyo, Kocha Nabi amekuwa na mzuka baada ya vijana wake kuliamsha mazoezini wakiwa salama baada ya awali kuugua ghafla mafua na kulazimika baadhi yao kucheza hivyo hivyo katika mechi yao na Tanzania Prisons na kushinda mabao 2-1.

Yanga iliyojichimbia kambini Avic, Kigamboni inajiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara utakaopigwa leo Jumapili saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.