Home Habari za michezo FT: SIMBA 2-0 WYDAD…..ONANA KAMA RONALDO…..BADO POINT HIZI SIMBA AFUZU….

FT: SIMBA 2-0 WYDAD…..ONANA KAMA RONALDO…..BADO POINT HIZI SIMBA AFUZU….

FT: Simba 2-0 Wydad

BAADA ya kumaliza kipindi cha kwanza cha ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0, dhidi ya Wydad Casablanca, Simba imefanikiwa kuweka rekodi tofauti tofauti.

Kwanza ndio imekuwa timu pekee kutoka Tanzania kumaliza kipindi cha kwanza cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa inaongoza msimu huu kwenye hatua ya makundi.

Vilevile imekuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kwenye michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo wa hatua ya makundi.

Pia kiungo mshambuliaji Andre Onana ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kutoka timu ya Tanzania katika michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza.

Timu nyingine inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kutoka Tanzania ni Yanga, ambayo itacheza kesho na Medeama saa 10:00 kwenye Uwanja wa Mkapa

Aidha kwa ushindi huo, Simba sasa inahitaji ushindi wa mechi mbili zijazo ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu robo fainal ya klabu bingwa Afrika.

SOMA NA HII  KISA KUWA WANIGERIA...OKWA NA AKPAN WAACHWA NA SIMBA...ISHU NZIMA IKO HIVI...