Home Uncategorized SABABU YA AZAM FC KUCHEZA TRANSIT CAMP YAFAFANULIWA KITAALAMU NA CIOABA

SABABU YA AZAM FC KUCHEZA TRANSIT CAMP YAFAFANULIWA KITAALAMU NA CIOABA


ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa uongozi ulipendekeza kucheza na timu inayoshiriki Ligi Kuu Bara ila ilishindikana kutokana na kila timu kuwa na program zake jambo lililofanya achague kucheza na Transit Camp.

Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuchezwa leo majira ya saa moja kamili usiku Uwanja wa Azam Complex.

“Baada ya siku saba za mazoezi, tumejaribu kuleta timu moja kwa ajili ya mchezo wa kirafiki, meneja wangu alitafuta timu nyingine ya ligi kuu, lakini kila timu ilikuwa na programu.

 “Nimependelea timu ya Transit Camp kwa sababu ilikuwa kwenye mipango yetu ya wiki,kupitia mchezo wetu huu wa kirafiki nina amini tutajua aina ya kikosi ambacho ninacho wa sasa,” amesema.

Juni 14, Azam FC itakuwa na kibarua cha kumenyana na Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  KIBABAGE WA MTIBWA SUGAR AMFUATA SIMON MSUVA DIFAA HASSANI EL JADIDA